emblem

Tanzania Standard Newspapers

TSN na PSSSF Wakutana Kujadili Biashara


TSN na PSSSF Wakutana Kujadili Biashara


TIMU ya Biashara ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) imekutana na wenzao wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF mjini Dodoma kwa lengo la kujenga mahusiano katika biashara pamoja na kuona namna watakavyoshirikiana kutoa elimu kwa umma.

TSN iliongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara, Soter Salema huku PSSSF ikiongozwa na Meneja Uhusiano na Elimu kwa wanachama, Omega Ngole. 

Washiriki wengine katika kikao hicho kutoka TSN ni Meneja Utawala na Rasilimali Watu, Siku Baleja na Meneja Mauzo na Usambazaji, Jonathan Manhe.